Friday, March 9, 2012

KAJEMBE: MZALAMO ALIYEUTEKA MJI WA MOSHI KWA MIHOGO.

Kila ifikapo jioni majira kama ya saa 10 hivi, baadhi ya Wakazi wa Mjini Moshi wanakuwa katika harakati ya kwenda mahali kujipatia chakula wakipendacho. Chakula hiki kimetokea kuwavutia wengi sana ambao hata hapo awali walikuwa wakiamini yakwamba ulaji wa mihogo ni hatari sana.
Hofu hii ilitokana na baadhi ya wenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro hususani Wachaga, kuamini kuwa mihogo ni sumu na si chakula, lakini siku hizi mihogo inalika kwa wingi katika Mji huu wa Moshi bila kuchagua Kabila la Wachaga, Wapare, Waarusha, Wazungu ama wanaotoka Asia.
Mihogo ikiwa jikoni katika eneo ambalo Mzee Kajembe anafanyia biashara.....Kajembe Shop.
Mmoja wa Vijana wa Mzee Kajembe, Mohamed ally.......akiweka mihogo jikoni.
Mzee kajembe, akitayarisha mihogo hiyo kwa kumenya.
Mzee Kajembe, akiwa na kijana wake Juma Kajembe......wakimenya mihogo.

Asikwambie mtu Moshi mihogo inaliwa.......hii ni foleni ya wateja wakisubiri mihogo.
Vijana hawapendi tena Chips Mjini Moshi, ni mihogo tu kutoka kwa Mzee Kajembe.
Hata Warembo nao hupenda mihogo ya Mzee Kajembe. Mdau nakusii ufikapo Mjini Moshi usiache kufika New Street jirani na Hoteli maarufu za Zebra na Buffalo, ili ujipatie mihogo ya aina yake.

- Picha na Habari na Mkuu Mroki a.k.a Father Kidevu.

No comments:

WATEMBELEAJI