Saturday, February 6, 2016

BUTIAMA...TULIVYOPOKELEWA KWA UPENDO MKUBWA SANA NA FAMILIA YA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE.


 Nikiweka taji la maua katika kaburi la Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.







Chai ya asubuhi pamoja na wadogo zangu nilioenda nao.

Kwakweli tulikaribishwa vizuri sana, kwa upendo mwingi sana sanaaa...rafiki yangu Madaraka Nyerere, ambae alinikaribisha kwenda kutembelea na kujua historia kamili ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere. Alitutembeza na kutupatia historia yote ya Baba wa Taifa, mpaka hatukuamini kwa ukarimu aliotupatia.....kwakweli tulijifunza mengi sana kuhusu Baba wa Taifa....na ni kweli Baba wa Taifa, maana anastahili kisawasawa kwa historia tuliyoipata.  Tulifurahi sana mimi na wadogo zangu, na lilikuwa jambo zito na la heri sana.
Mimi tulitaniana sana na Madaraka kila mara, hasa pale tulipoingia kunywa chai au kula, kila mara aliniweka kiti kikuu. '' Kwanini unaniweka kiti kikuuu, alijibu; kwasababu utakuwa DC siku zijazo. Pia hicho kiti wamekalia watu wakubwa sana kama; Mandera, Mseven, Mkapa, Kikwete, nk......hivyo na wewe unaandaliwa, anza kukalia hicho kitu ili ujiwekee baraka, alisema hivi....lakini kwa utani tu. Kwakweli tulifurahi sana sanaaa na kujifunza mengi sana haswa swala zima la kujali watu wotee na kupendana sana kwa ukarimu mkubwa. Sisi ni watu wadogo sana lakini tulipokelewa kama wafalme fulani......mimi binafsi nimejifunza sana kuheshimu wenzangu, binadamu wenzangu.....hata kama na mapungufu yangu lakini nilijifunza upendo na kusamehe wenzangu pale wanaponikosea.
- Kwakweli Mwalimu Nyerere anastahili sana kuwa Mwenyeheri ( Mtakatifu), maana nilijifunza na kuona mambo mbalimbali hapo Butiama anastahili kabisaaaaa!!!!!! bila wasiwasi.

Eee Baba wa Taifa, uhuko uliko uzidi uzidi kutuombea sisi Taifa lako, tuzidi kuwa na amani na upendo daima, kama ulivyokuwa ukisisitiza na kutufundisha daima mambo ya upendo, nasi tunakuombea sana tuuu.
Kwasasa nafikiri utakuwa umeipata hii kuwa tuna Jembe la nguvu Magufuli, anafuata nyayo zako kwa kishindo.....hebu jaribu kumwombea huko kwa Mungu, amlinde na mafisadi, wenye kutaka ubinafsi na mengineyo mengi tu. Ili ampe afya njema azidi kutuongoza vizuri daima bila kuogopa mtu yoyote. Basi kwa hayo nisikuchoshe sana, mengi unayafahamu na kuyaona....endelea kutulinda tu ili upendo wetu na amani yetu izidi kutawala daima Tanzania. Basi endelea kupumzika kwa amani Baba wa Taifa Mwalimu wetu Nyerere. Amina!

No comments:

WATEMBELEAJI