Saturday, August 27, 2016

MILA YANGU HII NAIKUMBUKA SANAAA...WAKATI WA KUPELEKWA SUNA. KWASISI WANYAMBWA WAGOGO, HAWA TUNAWAITA; WANYAMULUZI.

Enzi hizo za utoto wakati wa kupelekwa suna ili kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo mwanaume kwa baadae aje kuwa na familia njema. Lazima mwende kuishi porini kwa muda wa mwezi mzima, ili kujifunza utu uzima, ili baadae unapokua iwe msaada kuendesha familia....tulikua tunaona kama mateso sana kukaa porini kwa mwezi mzima, lakini kumbe ni faida sana kwa mafundisho mbalimbali ya kimaisha. Kwakweli nasikitika sana utamaduni huu unaanza kupungua sana, tunakoelekea utaisha kabisa, ni kosa kubwa sana hili. Mimi binafsi nilijifunza mengi sana hivyo najivunia utamaduni huu.
Sisi Wanyambwa-Wagogo tunaita Ikumbi, na vijana wenyewe wahusika wanaitwa Wanyamuluzi.

No comments:

WATEMBELEAJI