Saturday, October 9, 2010

NI:JUMAPILI YA ISHIRINI NA NANE YA MWAKA C.

Ni; Jumapili ya ishirini na nane ya mwaka C.
Insha: Wale kenda wako wapi?
Masomo: 2 Wafalme 5:14-17; 2 Tim 2:8-13; Luka 17:11-19.


Kiini cha masomo ya Jumapili hii, hasa ni muhimu wa kumshukuru Bwana kwa yote anayotufanyia daima. Ibada ya kila Jumapili yaani adhimisho la Ekaristia maana yake kutoa shukrani zetu kwa yote Mungu aliyekamilisha katika Kristo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwa kutuletea Utakatifu.
Hatuna budi kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa yote aliyo tujalia katika wiki hii, hata kama hatutapata nafasi ya kwenda Kanisani kwasababu mbalimbali zinazo tulazimu tusiende...Lakini inatubidi tusimame walau kidogo na kusema; asante sana Mungu Baba kwa uhai unao tupa, tukikumbuka uhai huu tulio nao ni mali yake na mambo yote tulio nayo ni mali yake.
-ASANTE SANA MWENYEZI MUNGU KWA MEMA YOTE UNAYO TUJALIA.

No comments:

WATEMBELEAJI