Monday, October 11, 2010

UTANDAWAZI TUJITAHIDI KUUTUMIA VIZURI!

Dunia tuliyonayo sasa kila siku inabadilika kwa kasi sana na tumefikia kwenye UTANDAWAZI.
UTANDAWAZI na Mama, UTANDAWAZI na Baba, UTANDAWAZI na Dada, UTANDAWAZI na Kaka, UTANDAWAZI kwa watoto, vijana, wazee wote ni UTANDAWAZI tu!
Tumerahisisha sana mambo yanakwenda fasta fasta kwa kupitia huu UTANDAWAZI, pia tumefanya dhambi nayo iongeze kasi kwa kupitia huu UTANDAWAZI.

Dunia imeongeza kasi sana, maarifa mengi yameongezeka kama watu wapendavyo, mawasiliano ya simu sasa ni rahisi sana, computer nazo zinazua mambo kila kukicha, mambo ni UTANDAWAZI tu! kila kukicha.

LAKINI TUKUMBUKE;

UTANDAWAZI huu tuutumie vizuri, tukiutumia vibaya hatutaiona Mbingu, wengi wetu wanatumia kwa Uzinzi, Ujambazi, ndoa nyingi zinavunjika, dhambi zimerahisishwa sana kwa njia hii ya UTANDAWAZI. Changamka ewe ndugu usije ukaangamia, tumia vyema huo mtandao wako, maana shetani nae anautumia sana ili apate wafuasi wengi. Jitahidi sana kuutumia vizuri huu UTANDAWAZI.

No comments:

WATEMBELEAJI