Monday, April 9, 2012

NDEGE YA ATCL YAANGUKA LEO ASUBUHI MKOANI KIGOMA!



Abiria 35 na Marubani waliokuwa wakisafiri na Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wamenusurika kufa baada ya Ndege waliokuwa wakisafiria kuanguka mapema leo asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
Ndege hiyo inadaiwa kupata dhoruba hiyo muda mfupi baada ya kushika kasi ya kutaka kuruka na kushindwa kufanya hivyo na kuanguka, lakini Rubani wake alifanikiwa kuituliza chini salama katika nyasi bila kuleta madhara makubwa.

No comments:

WATEMBELEAJI