Monday, April 9, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE.....ATOA ZAWADI YA PASAKA SUKAMAHELA!

Rais Jakaya Kikwete, atoa zawadi ya Pasaka kwa Wazee wa Kambi ya Sukamahela, Wilayani Manyoni.

Katibu Tawala Mkoa Singida, Mh.Liana Hassan (kulia) akikabidhi mbuzi watatu wakiwa ni zawadi kutoka kwa Rais Kikwete, kwa Wazee wasiojiweza wa Kambi ya Sukamahela, Wilayani Manyoni.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Mh.Liana Hassan (kulia) akikabidhi dumu la mafuta ya alizeti, moja ya zawadi zilizotolewa na Rais Kikwete, kwa Kambi ya Wazee wa Sukamahela.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida (kulia) akimvisha shati mmoja ya Wakazi wa Kambi ya Wazee ya Sukamahela.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Mh.Liana Hassan......akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete, kwa wakazi wa Kambi ya Wazee ya Sukamahela, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Bi.Fotunata Malya.

Mkazi wa Kambi ya Wazee wasiojiweza ya Sukamahela, Wilayani Manyoni....Bibi Kareudia Madoli, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake kwa Rais Kikwete kwa msaada wake kwa ajili ya sherehe ya Pasaka.

- Picha na Nathaniel Limu.

No comments:

WATEMBELEAJI