Monday, September 26, 2016

DADA WA SHOKA HUYU, HATAKI UTANI KABISA....ANAPIGA BASI SI MCHEZO, TENA BASI GUMU AINA YA SCANIA LENYE GIA NYINGI. RUTI ZAKE NI DAR - TUNDUMA!

Akina dada hawataki utani kabisa, nasikia huyu dada yupo vizuri sana barabarani, na ni safari ya mbali sana anayoifanya Dar es salaam to Tunduma. Si mchezo akina dada wasasa, hongera sana dada kwa uhasiri huu....maana fujo za barabarani ni nyingi mno, sasa wewe unastahili pongezi nyingi mno.

Tuesday, September 13, 2016

CHEKA UNENEPE KIDOGO!


FAMILIA YA WATOTO WENGI...TIMU KABISA YA MPIRA WA MIGUU!

Mshirikishe Mungu kwa kila jambo ana faida sana, akili za kibinadamu tu bila msaada wa ki-Mungu hakuna lolote. Ila kutimiza agizo la kuzaa nawapa hongera sana!

Watoto wote hawa ni wa bwana Irineu Cruz na mkewe Jucicleide Silva, wako 13 kama mnavyo waona kwenye picha hii.
Wanasema kwa miaka 20 wamekua wakijaribu kupata mtoto wa kike, lakini hawajafanikiwa na hivyo sasa wanasema; mpaka kieleweke wataendelea tu kujaribu hadi pale watakapo pata binti......watoto wao hawa wote wa kiume tayari wametosha kuwa timu ya mpira wa mguu ya kanda kabisa!

AFRIKA IWE NA SHUKRANI KWA JULIUS NYERERE ''ROBERT MUGABE''.

Afrika iwe na shukrani kwa Julius Nyerere, nataka Wazimbambwe wasimame kwa ajili ya Nyerere. Maneno ya rais wa Zimbabwe, '' Mh.Robert Mugabe''.

WATEMBELEAJI