Tuesday, September 22, 2009

BASI LA ABILIA LAWAKA MOTO KATI YA SINGIDA NA DODOMA.








Nikiwa njiani kutoka Mwanza kwenda Dar, nimekutana na ajali ya moto la basi la abilia kutoka Singida kwenda Dodoma. Lilipata hitilafu ya umeme na tairi, hivyo kusababisha moto huo. Kwa bahati njema abiria walikuwa chini ''wakichimba dawa'' lakini dreva wa basi hilo alikuwa akichungulia chanzo cha moto huo ndipo ghafula tairi liliasuka na kumjeruhi usoni, amekimbizwa hospiali ya Manyoni kwa matibabu.
Polisi walifika kwa kuchelewa kwenye tukio hilo ingawa simu zilipigwa mapema mno, na hata hivyo polisi hao walipofika walikuwa wamesheheni silaha kali bila kuwa hata na ndoo moja ya maji kusaidia kuzima moto huo.
(NA EMMANUELY MGONGO).


No comments:

WATEMBELEAJI