Thursday, November 26, 2009

KICHEKESHO CHA LEO!

Jamaa mmoja alikamatwa na Polisi wa doria, kwa tuhuma za uzururaji. Kabla ya kupelekwa kituo cha polisi akaleta usumbufu kidogo, hata hivyo Polisi walifanikiwa kumfikisha kituoni. Alipofikishwa kaunta ya kituo, yule afande aliyempeleka akamwagiza askari wa kaunta ampe chai yake (ampige) mtuhumiwa. Yule askari wa kaunta akampa chai yake (akampiga) sana mtuhumiwa. Alipo maliza tu kumpiga, mtuhumiwa naye akaanza kumpiga askari. Alipoulizwa kwanini anafanya hivyo, mtuhumiwa akajibu '' NAMRUDISHIA KIKOMBE CHA CHAI''

No comments:

WATEMBELEAJI