Padre Donatian Mwampinzi (35) wa Kanisa Katoliki, mkazi wa Dar es salaam na Sista Anuarite Kafumu (40) kutoka Shirika la watawa Mbingu - Ifakara, Wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa miili iliyotambuliwa katika ajali kati ya gari lao na basi la abiria mali ya kampuni ya Hood, eneo la hifadhi ya wanyama ya Mikumi.
Ajali hiyo ilitokea jana Des 8. Gari hilo dogo lilikuwa likitokea Jijini Dar es salaam kuelekea mjini Mahenge, Wilaya ya Ulanga na basi la abiria likitokea Mbeya kwenda Dodoma na hivyo kugongana katika eneo hilo la hifadhi ya mbuga ya wanyama Mikumi, Wilayani Kilosa.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Morogoro, Ibrahim Mwamakula, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo mnamo Desemba 8, 2009. Majira ya 7:40 mchana, kwa kuhusisha Gari T 155 AXM aina ya Scania Bus, mali ya kampuni ya HOOD ya Morogoro lililokuwa likiendeshwa na Willson Mushi (53) mkazi wa Kimara, Dar es salaam. Kugongana na Gari T 828 BAZ aina ya Toyota Hilux Double Cabin mali ya Kanisa Katoliki.
Mbali na watumishi hao wa Kanisa hilo, wengine waliotambuliwa ni: Said Mustapher (35) Fundi Chuma , mkazi wa Tandika-Dar, na Seif Mohamed (60) Fundi selemala, mkazi wa Majumba sita, Ukonga-Dar, ambao wote wanne walifariki dunia papo hapo wakati ajali hiyo ilipotokea ndani ya gari hilo la Kanisa.
Kwa mujibu wa kamanda huyo wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa Gari dogo hilo lilikuwa likiendeshwa na Padre Mwampinzi ambaye alifariki papo hapo baada ya ajali hiyo kutokea, pia abiria wengine wawili waliyokuwa ndani ya Gari la Padre, kujeruhiwa vibaya na walipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito ya Mikumi.
Kamanda wa kikosi hicho, aliwataja majeruhi wa Basi hilo, Wolbedegiorgh Asghed (61) ambaye ni Muhabeshi na mhandisi wa Kurasini, Jijini Dar na mwingine ni Anist Malesa (49) mkazi wa Dar, ambaye pia ni mhasibu wa St.Mary ya Dar es salaam, ambao hadi jana hali zao zilikuwa zikiendelea vizuri.
Aidha Kamanda huyo wa kikosi cha usalama barabarani alisema kuwa hakuna kifo kilichotokea kwa abiria waliokuwa wakisafiri na basi hilo.
-Mungu aziweke Roho za marehemu hao mahali pema peponi. Amina!
No comments:
Post a Comment