Thursday, December 24, 2009

ASKOFU WA ZAMBIA AVULIWA UASKOFU.

Bwana Milingo alipokuwa Askofu.
Bwana Milingo akiwa na mkewe Maria Sung wakati wa harusi yao.


Aliyekuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Zambia, Askofu Mkuu Emmanuel Milingo 79, amenyang'anywa mamlaka ya uaskofu na Vatican.
Alitengwa mwaka 2006 kwa kuoa na kujaribu kuwatawaza mapadri na kuwa maaskofu. Kanisa hilo limesema imebidi kuchukua hatua za ziada kutokana na uamzi wake wa kuwatawaza baadhi ya mapadri kuwa maaskofu mwezi Julai, jambo ambalo hufanywa na Papa peke yake.
Paul Samasumu, msemaji wa Kanisa Katoliki la Zambia, amesema ''amevuliwa wadhifa wa uaskofu na sasa anaitwa Bw.Milingo''.
Bwana Milingo alimwoa mtaalamu wa tiba ya kutumia sindano tupu yaani (Acupuncturist) ambaye ni raia wa Korea ya kusini, na ndoa hiyo ilifanyikia Mjini New York, Marekani.


No comments:

WATEMBELEAJI