Hata mimi nakumbuka mafuriko ya mwaka 1998 ilikuwa ni kasheshe kwa kila kitu, hasa kwa kusafiri hasa huko vijijini, na watu wengi walipoteza makazi yao. Mara nyingi tulilazimika kuacha magari kando ya mito maana ilikuwa haiwezekani kukatisha mto kwa wingi wa maji, na tulivuka kwa miguu. Pia tulijaribu kusafiri na Trekta kwani Trekta lina nguvu kwenye tope na maji lakini haikuwezekana ilikuwa ni kukwama mtindo mmoja. Kwakweli mafuriko si mchezo, kwahivyo nawapa pole sana wote waliokumbwa na janga hili la mafuriko.
Maisha yanakuwa magumu sana, bidhaa hupanda bei sana na inakuwa vigumu sana kupata mahitaji mbalimbali.
Maisha yanakuwa magumu sana, bidhaa hupanda bei sana na inakuwa vigumu sana kupata mahitaji mbalimbali.
1 comment:
habari kaka. Nimependa picha zako za athari za mafuriko kwenye barabara za vijini. Hapo ni wapi na yalitokea tarehe ngapi?
Post a Comment