Wednesday, February 10, 2010

MADEREVA WETU WA DARAJA LA C NI WAKWELI?

Mafunzo ya udereva daraja la C; inamaanisha kuendesha basi, lori, gari ndogo, pikipiki. Je madereva wetu wa Tanzinia wenye daraja la C wanastahili kweli? Maana vituko tunavyo viona barabarani hasa kwa madereva wa mabasi, hadi inatokea balaa kubwa kwa ajali za kutisha. Mimi nafikiri wengi sana hawajapitia mafunzo haya, la sivyo isingelikuwa balaa kama tuzionazo, na hasa kupoteza ndugu zetu wengi kwa ajali zisizo za kawaida, kwa upuuzi tu wa hawa madereva ambao hawajapitia mafunzo kama haya. Ni mhimu sana kujifunza vizuri sheria za barabarani na kuzitumia ipasavyo, madereva wa mabasi tafadhalini nendeni shule, la sivyo mtaendelea kutumaliza tu!

No comments:

WATEMBELEAJI