Mwaka juzi, nikiwa na mdogo wangu na rafiki yetu tukitokea Dodoma kuelekea Dar es salaam, hapo ndipo tulipo shuhudia ajali hii ikitokea, maeneo ya Dakawa. Basi la SHABIBY lilipo chinja ng'ombe zaidi ya kumi na tano (15) kwa mpigo, basi hilo lilikuwa likitoka Dar kuelekea Dodoma, hewezi amini kama unajua kuendesha gari ni maajabu sana jamaa aliweza kulikabili basi kisawasawa bila kuliangusha, ni kama miujiza vile. Mimi niliogopa na kupaki pembeni gari, na kushuhudia nini kitatokea, na nilisema lazima aanguke lakini bahati nzuri alibaki kasimama yaani kama utani, nilimsifu sana dreva mara mia moja, maana ilikuwa sikawaida. Toka nimeanza kuendesha gari na kusafiri barabarani hii ilikuwa ajali yangu ya nne kushuhudia live.
Tajili wa ng'ombe hao sio hao wamasai tunaowaona kwenye picha, bali ng'ombe walikuwa wakisafirishwa kutoka Mwanza kuelekea Dar, hapo Dakawa walikuwa wameshusha tu kwaajili ya kuchunga kidogo kabla ya kuendelea na safari yao, ndipo wahudumu wa hao ng'ombe wakajisahau na kuwaacha wakielekea barabarani, ndipo ng'ombe hao mauti yalipo wakuta, hadi huruma!
Siku hiyo ilikuwa ni sherehe kwa wananchi wa Dakawa, nyama bwelelee...!!!
Hapo angelikuwa Babu yangu mzaa Mama, na kapresha juuu!!! Maana alikuwa hataki kuchinja hata ka mbuzi tu, kwa ubahili na kupenda kuona mifungo wake na kujisifu tu mimi ni tajili ng'ombe nina ng'ombe wengi...mara hivi mara vile, lakini analala kwenye kitanda cha ngozi. Kazi kweli kweli.....!!!!!
No comments:
Post a Comment