Monday, March 29, 2010

MMILIKI WA LORI LILILOSABABISHA AJALI YA KIBAMBA AKAMATWA.

Kamanda Msika akiongea na waandishi wa habari.
Mmiliki wa lori lililosababisha ajali ya Kibamba atiwa nguvuni mpaka Dereva apatikane!!! Lori lililosababisha vifo vya watu 11, katika eneo la Kibamba darajani - Jijini Dar es salaam, Polisi wamemkamata mmiliki huyo aitwae Mohamed Mahamoud, na inasemekana amekuwa hatoi ushirikiano wa dhati ambao ungewezesha kukamatwa kwa Dereva Kudra Adam, ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo, na anayetuhumiwa kwa ajali hiyo ya kuuwa watu 11. Kamanda wa kikosi cha barabarani, Mohamed Mpiga alisema; huyu jamaa tumemkamata anakua anasitasita kutupatia ushirikiano ili tuweze kumpata Dereva wa lori hilo, nachukua nafasi hii kuwahakikishia ni lazima tumkamate na tutamuachia huyu mmiliki mpaka Dereva apatikane; alisema Kamanda.

No comments:

WATEMBELEAJI