Wednesday, March 3, 2010

RAIS KIKWETE AMUAGA MLINZI MKUU WA ZAMANI.

Rais JK, aliongoza waombolezaji katika kumuaga aliyekuwa mlinzi mkuu wa zamani, aliyehudumia marais wawili Tanzania, David Simbeye (77) aliyefariki dunia jumapili iliyopita. Alikuwa mlinzi mkuu wa marais Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Misa ya kumuaga marehemu Simbeye ilifanyika Dar es salaam nyumbani kwa mtoto wake Leonard Simbeye, Kijitonyama ambapo viongozi wengine nao walishiriki.
Baadhi ya viongozi wengine waliohudhuria katika kuaga mwili huo ni; Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mzee Mwinyi, mjane wa Baba wa Taifa mama Maria Nyerere, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Waziri wa maji na umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya.
Akisoma wasifu wa marehemu baada ya misa, mwakilishi wa familia Adam Simbeye; alisema Simbeye wakati wa uhai wake alifanya kazi yake katika Idara mbalimbali za Jeshi la Polisi nchini akiwa mchapakazi na mwadilifu.
Alisema akiwa mtumishi wa Ikulu wakati wa uhai wake, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali na kwamba alikuwa kiongozi wa kikosi cha ulinzi na usalama wa Taifa. Simbeye alistaafu kazi mwaka 1988.

-Mungu ailaze mahali pema peponi Roho ya marehemu Simbeye. Amina!

No comments:

WATEMBELEAJI