Wednesday, March 24, 2010

WANASIASA WAVUA NGUO KUPINGA BAJETI-ROMA.

Wanasiasa wa Jiji la Roma - Italia, wakionyesha nguo zao za ndani walipokuwa wakipinga sera ya Gianni Alemanno (Meya wa Jiji hilo la Roma) aliyegoma kupitisha bajeti ya Jiji hilo.

Katika kile kinachoonyesha sasa wanasiasa wa nchi ya Italia wamecharuka kwelikweli kwa kutaka maendeleo, hivi karibuni maofisa wa Manispaa wa Jiji la Roma walikusanyika na kufanya maandamano kwa kuvua suruali zao wakilazimisha kupita kwa bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka 2010. Moja kati ya bango walilokuwa wamebeba lilisomeka ''maeneo ya kupaki na bustani zimevunjwa watu hawana makazi''.
Meya Sandro Medici wa Cinecitta, nje kidogo ya Roma, alimtaja mwanasiasa ambaye ni Meya wa Roma Almanno aliyekataa kupitishwa kwa bajeti hiyo kutokana na kudai kuwa na kodi ambazo sio za msingi.

-Kwa sasa siasa ya Italia kwakweli imeyumba sana, na mambo mengi sana hayaendi vizuri kama ipasavyo, ugomvi kila mara kwa wanasiasa kutokana na hali mbaya ya kiuchumi na mambo kedekede si ya kawaida.

No comments:

WATEMBELEAJI