Jana katika kushangaa kidogo Mamiss watarajiwa wa Italia wakiandaliwa kwa shindano la mwaka huu, akiwemo rafiki yangu, aliye nialika nikamshuhudie. Huwa najiuliza sana sipati jibu, Mamiss Duniani wanasaidia nini??? Nikamuuliza hata huyo rafiki yangu akajikanyaga kanyaga wee kunipa jibu sahihi...ameshindwa, mara oh... wawapendezeshe watu kwa urembo, bla bla blaaa....!!!!! nyingi bila kunipatia jibu sahihi. Inaonekana hata washiriki wengi wa kuwa Mamiss hata wao hawajui maana yake nini kuwa Miss.
Kazi kweli kweli!!!!
1 comment:
Naona maswali ni mengi lakini majibu ni zero.Hapa ni biashara tu na zaidi ya habari hakuna.Huu ni ulimwengu wa biashara na kila mtu kwa hiari yake anaweza kufanya ili mradi jamii ipo kwa ajili yake.Kupitia mashindano haya watayarishaji na wadhamini wao kwa pamoja wananufaika sana kiuchumi na hao washiriki kwa upande wao huvuna walichopanda.
Post a Comment