Thursday, May 13, 2010

KIBAKA ANAPO CHOMWA MOTO!

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ali Kumbenda ( Kwenye video hii), alipo uwawa kinyama na watu wenye hasira kali, mbele ya Polisi kwa tuhuma za kutaka kupora pikipiki waliyokuwa wameikodi kutoka Mkuranga kuelekea Chanika Wilaya ya Ilala - Jijini Dar es salaam.

- Damu yake itawalilia, pikipiki tuu...haina thamani kuliko roho ya mtu. Kuua mtu ni dhambi kubwa, pia Polisi alikuwepo anashuhudia kabisa, kwakweli hafai katika kazi hiyo ya upolisi. Mtu kama ameiba anatakiwa apelekwe mbele ya sheria na apewe adhabu ya kifungo na kadhalika si kuchukua jukumu zito kama hili la kumuua kwa kumchoma moto, we ni nani mpaka umhukumu mwenzio kifo? Umekamilika kikamilifu kwa yote?? Je kama wale wanaoiba pesa za Serikali ambayo ni makosa makubwa zaidi, wale Polisi wanaoiba pesa kwa rushwa, yaani wangehukumiwa hivi; wale mapapa na manyanumi, wangekuwa wanachomwa moto, je nani angebaki?

No comments:

WATEMBELEAJI