Kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua katika maeneo ya Pwani - Morogoro na Mikoa mbalimbali Nchini, hali ya barabara hasa zisizokuwa na lami zinaharibiwa vibaya na kusababisha kunasa (kukwama) kwenye matope kama ilivyokuwa katika barabara hii ya Lupiro - Malinyi eneo la Liwambanjuki, kama tuonavyo hapo kwenye picha magari haya yenye Four Wheel yakichemka kwa kukwama, magari haya ni ya msafara wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakielekea katika shughuli mbalimbali za Jamii, yakiwa yamezama katika eneo hilo na kuchukua zaidi ya saa mbili hivi kujinasua na kuendelea na msafara huo.
-Mdau John Nditi wa Morogoro.
1 comment:
Duh! pole sana, hapo ndipo utakapoona mwanaume analengwa na machozi. Maisha haya jamani kaziiiii kwelikweliiiii.
Post a Comment