NATAFSIRI KIDOGO WIMBO HUU; Mpendwa Yesu nakuandikia, kwasababu hakuna anae kuandikia, kwasababu mioyo yetu ni kiziwi haisikii na mioyo imetawalwa na maovu, kwa yule anae kusaliti na ndoto zake ambazo hazina naana, hazina msaada wa kusaidia wengine. Mpendwa Yesu nakuandikia kwa ajili ya yule ambaye hana nyumba, katoka Afrika mbali kutafuta maisha na hana makao maalum, umsikilize na kumsaidia, kwani watu hawasikii tena upendo wako wa kuwapenda wengine.
UJUMBE WA LEO!
-Ingawa mimi napendeza, ingawa wewe wapendeza, kupendeza si kitu. Ingawa mimi najipamba, ingawa wewe wajipamba, kujipamba kwa miili si kitu, kujipamba kwa mavazi bila matendo mazuri ni bure tu! wajidanganya tu! Uzuri wa uso wangu, uzuri wa uso wako bila Mungu ni bure tu! Wingi wa mali zako bila Mungu ni bure tu! Uzuri watoka kwa Mungu, mali yatoka kwa Mungu, na majivuno yako yote bila Mungu ni bure tu! Kumbuka kila mtu kaubwa kwa jinsi yake hivyo kila mtu ana thamani, awe maskini, kilema, kipofu, n.k watu wote wana thamani.
Wengi wajisifia kwa maneno ya watu, wanapambwa kila kona kwa maneno mazuri bila kufikiri - na wewe wajiona mzuri mpaka kufikia kusahau maagano ya Mwenyezi Mungu, kwa kusifiwa sifiwa tu!
Uzuri ulionao mshukuru sana Mungu, mali uliyonayo mshukuru sana Mungu bila kujisifia sifia na kutaka kusifiwa na watu. Uzuri ni karama toka kwa Mwenyezi Mungu, tumia uzuri wako kumshukuru Mwenyezi Mungu aliye kupatia hivyo, na kuwajali watu wote.
JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NINYI NYOTE WADAU WANGU!
1 comment:
weekend njema na jumapili njema kwako pia na asasnte kwa wimbo pia ujumbe nimependezwa sana.UPENDO DAIMA.
Post a Comment