Monday, June 21, 2010

YARABI! KOMBE LA DUNIA LASABABISHA KIFO.

GREENPOINT STADIUM, CAPETOWN - SOUTH AFRICA.
Wakati fainali za Kombe la Dunia zikiendelea, huku familia kadhaa zikishangilia kuwepo kwa msimu huu wa soka, familia nyingine ni vita kubwa endapo hakuna uwezekano wa kuwepo kwa Televisheni ya pili.
Suala hilo limejidhihirisha kwenye familia moja huko Nchini Afrika ya Kusini, yenye maskani yake katika kijiji kidogo cha Makweya, baada ya Baba wa familia hiyo aliyejulikana kwa jina la David Makoeya, kupigwa hadi kufa na mkewe ambae ameshirikiana na watoto wake wawili. Sababu kubwa ya mkasa huo ni kufuatia Baba huyo wa familia hiyo mwenye umri wa miaka 61, kutaka kuangalia mchezo kati ya Ujerumani dhidi ya Australia, familia yake ilikuwa ukumbini ikifuatilia kipindi cha nyimbo za kwaya.
Akieleza mkasa huo Polisi anayeshughulikia kesi hiyo Mothemane Malefo, amesema; kufuatia marehemu David kutaka kutazama mpira ilimlazimu kuchukua ''Rimoti'' na kubadili channel hatua ambayo ilichukiza familia yake na kuanza kupigwa.
Amesema wakati zogo hilo likiendelea majirani wa familia hiyo walipiga simu Polisi na kwa bahati mbaya walipofika eneo la tukio walikuta tayari David Makoeya ameshafikwa na mauti.
-Wavuti.

No comments:

WATEMBELEAJI