Friday, July 2, 2010

HATIMAE MAFUNZO YA WIMBO WA KISWAHILI YAMEISHA LEO!

Hatimae yale mafunzo ya wimbo wa Kiswahili niliyokuwa nikiwafundisha wanafunzi wa shule afundishae rafiki yangu Isabella, yameisha leo na kesho ndo sherehe yenyewe....sasa sijui itakuwaje, ngoja tuone kama wataimba vizuri hawa watoto. Lakini wapo kamili sasa, nimefurahi sana kwa bidii yao waliyo onyesha katika kujifunza wimbo huu. Mara baada ya sherehe nitawaleteeni video ya wimbo huo, kama nikiweza kuchukua...maana pia mimi ni mpiga ngoma wao, kazi kweli kweli....!!!

1 comment:

ray njau said...

Jitahidi tu kwa kuwa tunaisubiri kwa hamu sana.Ni kazi tu.

WATEMBELEAJI