Wednesday, September 29, 2010

NIKIWA MWITONGO - BUTIAMA KWA MWALIMU NYERERE!

Mkuu Madaraka, mtoto wa Mwalimu Nyerere; akinionyesha sehemu ya kusaini kitabu cha wageni.





Nikianguka sahihi katika kitabu cha wageni, waendao kutembelea nyumbani kwa Mwalimu Nyerere.



Mkuu Madaraka, mtoto wa Mwalimu Nyerere ndani ya maktaba ya vitabu vya Mwalimu.




Tukishangaa wingi wa vitabu alivyo visoma Mwalimu na vingine alivyo viandika yeye mwenyewe wakati wa uhai wake. Vitabu vyote vilivyopo hapo amevisoma, huwezi amini ni vingi mno zaidi ya 8000.





Mbele ya kaburi la Mwalimu tukisali na kutoa heshima zetu.






Nikiweka shada la maua katika kaburi la Mwalimu Nyerere.








Pamoja na Madaraka Nyerere, mtoto wa Mwalimu. Mbele ya kaburi la Baba yake Mwalimu Nyerere.







3 comments:

Mbele said...

Shukrani sana kwa taarifa hii na picha. Sasa najiuliza, hao vigogo wetu wa leo wana vitabu majumbani mwao? Wanasoma vitabu?

Nimepata changamoto kubwa kusikia kuwa Mwalimu alikuwa na vitabu vingi namna hiyo. Nadhani taarifa ya aina hii niliiona pia kule kwenye blogu ya Madaraka Nyerere.

Vitabu 8000 si mchezo. Mimi ninakisia ninavyo 3000, na nilikuwa nadhani ni vingi sana! Itabidi nifanye juhudi ili angalau nifikie nusu ya hivi vya Mwalimu.

Baraka Chibiriti said...

Asante sana mh.!

Madaraka said...

Baraka, hiyo picha moja naonekana kama nimelala usingizi!

WATEMBELEAJI