Hapa kwa ndani ni makumbusho ya Mwalimu Nyerere, unapata maelezo mazuri sana na kuona nguo na vifaa mbalimbali alivyokuwa akitumia Mwalimu.Nilishituka sana baada ya Madaraka kuniambia; Hicho kiti ulichokalia unajua wamekalia akina nani? Akaanza kuwataja. Kiti cha heshima sana!

Hapa tukiwa Mwitongo - Butiama, tukianza safari ya kurudi Dodoma.
Mchuma wangu (Kachumba kangu), usiudharau kabisa! We kaone kamechakaa tu lakini kapo fiti sana...kalipiga tripu ndefu sana; Dar to Dodoma - Singida - Shinyanga - Mwanza - Musoma - Butiama (Mwitongo). Na kurudi bila shida kabisa, wenye mashangingi yao hawakuamini kabisa, hasa rafiki yangu mmoja alikataa kabisa kama nimesafiri na kakibelenge haka. Na kunitania kwa sana, lakini ndo hivyo...ni gari yangu ninayoitegemea TZ.
No comments:
Post a Comment