Sunday, September 12, 2010

USHINDI WA KISHINDO WA CESENA DHIDI YA AC.MILAN JANA USIKU.

Amini usiamini timu ndogo kama ya Ac.Cesena, ambayo imepanda daraja mwaka huu bado changa kabisa. Jana usiku iliipa kipigo timu kongwe ya Ac.Milan kwa kuibuka kwa ushindi wa mabao mawili bila. Mchezo huo ulichezwa jana usiku 20:45 katika ligi kuu ya Italy (Serie A). Nilishuhudia mpambano huo katika uwanja wa Dino Manuzzi mjini hapa Cesena. Niliona Ac.Milan kuzidiwa sana na kushambuliwa vya kutosha. Zote mbili ni timu zangu za ushabiki nchini hapa Italy. Hongera sana Cesena!!!

No comments:

WATEMBELEAJI