Sara Pretto, akiwa Miyuji - Dodoma, Tanzania katika kituo cha masista wa jimbo la Dodoma cha kulea watoto walemavu wa akili.
Furaha ilioje baada ya kutembelea Tanzania na kusaidia kituo cha watoto walemavu cha Miyuji - Dodoma. Mdada Sara na wenzake wawili kutoka hapa Italia- mji wa Verona, wamerudi hivi karibuni kutoka huko Dodoma na kunihadisia mambo mengi mazuri, waliyo yafanya kwa watoto walemavu wa akili wa kituo cha Miyuji, karibu sana na ninapo kaa mimi. Nimeongea na Sara na amenitumia baadhi ya picha za huko. Amesema anapenda sana arudi tena, ikiwezekana upesi sana maana amepata upendo mkubwa sana kutoka kwa watoto hawa na watanzania kwa ujumla. Ni jambo la kufurahi sana.

-Asante sana Sara na wenzio kwa upendo wenu kwa watoto hawa!
No comments:
Post a Comment