Sunday, October 17, 2010

NJOONI WOTE TUMSIFU MAMA YETU MPENDWA MARIA!

NJOONI TUMSIFU MAMA YETU MPENDWA MARIA KATIKA MWEZI HUU WA ROZARI WA MARIA.

-Kama Mkatoliki mwezi huu wa Oktoba ni wa sala ya Rozari Takatifu, tukimkumbua Mama yetu mpendwa Maria. Ili azidi kutuombea kwa Mwenyezi Mungu kwa mambo mbalimbali ya hapa Duniani, hasa kuwa na Amani na mapendo zaidi.


Njooni wote tumsifu Mama yetu mwema, Mama yake Mkombozi, Mama asie na doa, chombo bora cha Ibada. Mama mwombezi wetu atuombea kwa Mungu, nchi iwe na Amani, machafuko yasiwepo atuombee kwa Mungu. Tunapo sali Rozari atuombea kwa Mungu, wote tumshangilie Mama yetu mpendwa, vigelegele tupige, makofi tupige, kayamba nazo tupige, tumshangilie Mama!

Twakuomba sana Mama yetu uiombee Tanzania, tuombee kwa mwanao ailinde Tanzania, vurugu za kisiasa zisiwepo Tanzania, machafuko ya kidini yasiwepo Tanzania. Hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu. Tunajiweka mikononi mwako Mama!

No comments:

WATEMBELEAJI