Wednesday, October 6, 2010

SIKU MARAFIKI ZANGU MOSES & MARISELDA WALIVYO MEREMETA!

Mbele ya Altare ya Mungu kwa ushuhuda wa pingu za maisha.


Furaha za marafiki wakiwarushia mchele baada ya kufunga pingu za maisha, wakitoka kanisani.



Pamoja na wafanyakazi wenzao.



Pamoja na ndugu wa Moses.




Kwa raha zao, kwa ishara ya upendo!





Keki keki keki kekiii, keki hiyoooooooo........!!!!!!







Pamoja na Paroko aliye wafungisha ndoa.






Pamoja na wanakwaya spesho kutoka Nigeria.







Tayari wamesha meremeta hapa. Nilikosekana mimi tu siku hiyo ya shangwe ya rafiki zangu Moses na Mariselda, lakini nilikuwa pamoja nao kwa sala, pia nilipiga simu kutoka Tanzania nyumbani ambapo nilikuwa likizo, bahati mbaya hakuweza kubadili siku, pia mimi sikuweza kubadili ticket kutokana nilikuwa tayari na ticket ya kwenda Tanzania, na kulikuwa na maswala mhimu sana huko Tanzania. Moses ni rafiki yangu wa kutoka nchini Nigeria, na Mariselda ni wakutoka Peru ni shangwe sana kwa kuungana kwao kuwa kitu kimoja.
Moses anasema kwangu; Bado wewe sasa!
Mimi namjibu hivi; Bado sijampata wangu wa moyo, nikimpata yule ambae ninampenda katika shida na raha. Milima - Nitapanda nae, Mabonde nitashuka nae. Nitajifunza Zeze ili limbembeleze, nitajifunza Gita nyuzi zimwite kwa kuvutiwa nami.
Acha acheke kwa maneno haya.









Pamoja na marafiki wa karibu.










1 comment:

ray njau said...

Naamini siku ipo,lakini siku haijafika.Ikifika ni shangwe kwa moyo na furaha kwa familia yako.Kumpata wa moyo wako,ni yule laazizi nyongo mkaa na ini.Kwa shangwe vigelegele nderemo na furaha bila kusahau vifo baraka na iwe juu yako baraka mwenye baraka.
-----------------------------------
N-D-O-A
NYUMBANI
DAIMA
OMBENI
AMANI
-----------------------------------

WATEMBELEAJI