Sunday, October 3, 2010

TARANTA TULIZOPEWA NA MUNGU TUZITUMIENI VIZURI!

Taranta tulizopewa na Mwenyezi Mungu tuzitumieni vizuri kwa kujipatia utimilifu na utakatifu.

Kama wewe ni Baba wa Familia au Mama wa Familia, kama wewe ni Kasisi Kanisani au Msikitini ni vema utimize wajibu wako vizuri ili upate ukamilifu vizuri.

Kama wewe ni Hakimu toa haki kamilifu, au kama wewe ni Askari tenda haki sawasawa usionee wanyonge maskini, acha rushwa, acha dhuruma, tenda haki vyema kwa watu wote ili utimize vema wajibu wako na ujipatie Utakatifu.

Kama wewe ni Daktari au Nesi hudumia wagonjwa wote kwa upendo, na mliopo mashambani, maofisini wajibika ipasavyo acha uvivu, fanya kazi kwa bidii ili utimize vema wajibu wako.

Tujitahidi sana kuzitumia taranta zetu ki ukamilifu na kwabidii ili siku moja tufanikiwe kuuona Ufalme wa Binguni na kukutana na Baba yetu mpendwa na kufurahi nae milele daima! Maana vitu na mambo ya Duniani ni yakupita tu!

No comments:

WATEMBELEAJI