Saturday, November 13, 2010

MR.EBBO NA WIMBO WAKE HUU TENA ANASEMA....

NIMEOA MREMBO MZURI...LAKINI HAJUI KUPIKA;

Nimeoa mrembo mzuri mjini, lakini hajui kupika! Analinga mrembo mzuri lakini hajui kupika kabisa, mrefu na mwembamba na mwendo wake kama twiga...lakini hajui kupika!Nifanyeje na mahali yangu imeshaliwa?
Nimeoa mtoto mzuri anatingisha mji, binti malidadi jamani na ninaye mpenda vyema, kufika nyumbani chakula mezani ugali wa unga wa mahindi, utasema wangano, mchuzi wa nyama ni bahari; chumvi imejazwa ngè! Akipika wali utasema kama kasonga ugali, tumbo linavuruga vuruga kwasababu ya chakula kibichi. Nimechoka Baba mkwe nirudishie mahali yangu leo, wageni wakija nyumbani naenda kununua chips, hata chai napika mwenyewe vinginevyo chai apikayo yeye hainyweki kabisa! Anachojua ni kuchemsha maji ya kuoga tu! kila siku anakata vidole anapo kata kata nyanya, kukuna nazi tu mpaka akaombe kwa majirani. Akipika pilau utazani mashudu ya ng'ombe....tumbo linavuruga vuruga sana!
Nimechoka Baba mkwe nipe mahali yangu leo!

-Kazi kwei kweliii...!!!!!!

No comments:

WATEMBELEAJI