Thursday, November 11, 2010

MR.EBBO... WIMBO WA KUCHEKESHA.ACHA HIYO TABIA MBAYA!

Nilinunua kanda ya Mr.Ebbo, jana nilikuwa nikisikiliza wimbo wake mpya unaochekesha sana, pia ni mambo ya kweli yanoyotokea karibu kila siku, mara kwa mara katika Jamii yetu. Jamaa kwekweli ana kipaji cha kutunga nyimbo na kuchekesha. Wimbo unasema Acha hiyo tabia mbaya;

Acha hiyo tabia mbaya;
Umepanda kwenye basi, hujui kuna nani unatukana tu ovyo ovyo!!!
Kuingia Ofisini kwa mtu hujaoga, unanuka kikwapa vibaya!!!
Ukitaka kumwuliza mtu kitu, husalimii unauliza tu eh!!!
Kutania dini za watu, unavaa kanzu unakwenda kwenye kitimoto eh!!!
Ukitoa sadaka unaweka mkono tupu tu...huweki hela yoyote Kanisani!!!
Umesema unataka kuoa, tukakuchangia hela ukafungulia biashara...hujaoa!!!
Kudipu dipu mtu, akikupigia huna la kumwambia!!!
Unaenda nyumbani kwa mtu umekunywa pombe mbovu mbovu, unanukisha nyumba nzima!!!
Unaazima kitu cha mtu, halafu hurudishi...kimekuwa ni chakwako!!!!
Unaomba omba pombe kwenye Baa we hununui, unasumbua watu tu!!!
Kumwita mtu kwa kabila lake, eti we Mpale njoo hapa!!!
Kuzarau zarau mabaamedi ( wauza baa) we mwanamke kuja hapa!!!
Wapiga debe kufutia futia nguo za watu, mnachafua watu bwana!!!
Unakwenda kwenye sherehe hujaalikwa, ukitolewa unarusha ngumi!!!
Mtu anafanya biashara, hakai kwenye biashara yake mpaka aitwe!!!
Unapiga mswaki, unakohoa vibaya na kutema kwa sauti!!!

ACHA HIYO TABIA MBAYA!!!

No comments:

WATEMBELEAJI