Sunday, November 14, 2010

NIKITAFAKARI UPENDO WAKO BABA MUNGU!....

Bwana asema; Mawazo ninayo wawazia ninyi ni mawazo ya amani wala si mabaya. Nanyi mtaniita nami nitawasikiliza, nami nitawarudisha kutoka mahali pote watu wenu waliofungwa;

Nikitafakari upendo wako Bwana, nikitafakari wema wako Baba Mungu, hakika wewe ndiwe mwenye huruma, ninapo tazama maisha yangu toka utoto wangu mpaka leo hii, nimefika hapa kwa neema yako Bwana, wala sikutenda lolote lililo jema sana. Uhai umenipa bure, uzima umenipa bure, watoto umenipa bure na mali umenipa bure bila kutenda lolote lililo jema. Wengine wanatamani wangekuwa wana mali hawajapata, wengine ni yatima, wajane, wengine ni vilema...nani awahudumie, wahurumie Ee Bwana. Uzima nilio nao mimi, sio kwamba nimetenda mema mbele za Mungu na vitu nilivyonavyo, wengine hawana si kwamba nimetenda mema sana mbele za Mungu. Mbona wapo walio tenda mema sana, Bwana mimi sikutenda njema, mbona wapo walio tenda mema. Ushukuriwe sana ewe Baba kwa wema wako, uhimidiwe ewe Baba kwa wema wako, uhimidiwe ewe Baba kwa upendo wako. Mimi ni nani Bwana mpaka unithamini,,,,nilikuwa na rafiki zangu tukicheza pamoja, lakini wametoeka, nilikuwa na jamaa zangu niliyo wapenda sana, lakini wametoeka....wema wako Baba na huruma yako kwangu mimi vyanishangaza. Tumrudishie utukufu Bwana, ni mengi sana Baba aliyo tutendea, astahili kuabudiwa, kuinuliwa daima, inatupasa kumshukuru daima. Asante sana Bwana kwa yote unayo tutendea!

Ee Bwana Mungu wetu, tunakuomba utujalie tufurahi daima katika kukutumikia wewe, maana kama tunakutumikia daima wewe Mwumba wa mema yote, tunayo heri iliyo kamili siku zote. Na vitu vyote tutapata kwa njia yako, kwa kukuamini wewe tu!

No comments:

WATEMBELEAJI