Friday, November 19, 2010

PANCHA NA MAUDHI YAKE UKIWA SAFARINI...


Pancha zinaudhi sana safarini, wewe unategemea na umepanga ufike saa fulani mahali uendapo, lakini mara pancha hiyoo...!!!! huwa ni maudhi sana na karaha kweli kweli, hasa kwa wageni. Na ukichukulia wenzetu hawajazoea mambo kama haya ya pancha kila mara.
Hapa ni mwaka jana, wakati tukitoka Singida kuelekea Arusha njia ya kati ya Babati. Tulipata pancha mara mbili, safari ikawa ya mafungu na mipango ikaharibika kidogo. Kwetu huwezi kupanga utafika saa ngapi na siku gani.

No comments:

WATEMBELEAJI