Sunday, November 28, 2010

TAFAKARI YANGU YA JUMAPILI YA LEO!

JUMAPILI YA KWANZA YA MAJILIO...KATIKA KUJIANDAA KWA KUZALIWA KWAKE BWANA WETU YESU KRISTU! KATIKA SIKUKUU YA X-MAS.


Sauti ya Mtu aliaye nyikani, itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake. Kila bonde litajazwa, na kila mlima na kilima kitashushwa. Palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patalainishwa, na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.


Ee Bwana nakuinulia nafsi yangu, Ee Mungu wangu nimekutumaini wewe nisiaibike milele, adui zangu wasifurahi kwa kunishinda. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja.

Tazama Mungu ndiye anaye nisaidia, Bwana ndie anayeitegemeza nafsi yangu.
Kwaukujufu wa moyo wangu nitakutolea dhabihu, Ee Bwana nitalishukuru jina lako siku zote!
Ee Bwana kwa jina lako uniokoe na kwa uweza wako unifanyie hukumu.
Ee Mungu uyasikilize maombi yangu, uyasikilize maneno ya kinywa changu!

-Nakushukuru sana kwa yote uliyo nijalia na kwa kunilinda na hatari zote kwa wiki hili zima nililo limaliza salama. Nakuomba sana unilinde tena kwa kuniepushia na hatari zote katika wiki lijalo, tunalo lianza sasa. Amina!

1 comment:

Anonymous said...

Utukufu, heshima na adhama vina YEYE (MUNGU) milele na milele kwa kuwa ndiye mmiliki

WATEMBELEAJI