Wednesday, February 16, 2011

DHULUMA NA MANYANYASO KWA WANAWAKE HAZINA NAFASI TENA!

DHULUMA NA MANYANYASO KWA WANAWAKE NA WASICHANA HAZINA NAFASI TENA! WATU WANAPASWA KUBADILIKA; .......

Wanawake wengi sana katika maisha yao wamekumbana na manyanyaso na vipigo ambavyo vinawavunjia haki na heshima zao, ni mambo yanayohatarisha pia afya na ustawi wa wanawake katika kuchangia maendeleo endelevu katika sekta mbalimbali za maisha.
Dhuluma na manyanyaso dhidi ya wanawake ni kinyume kabisa cha haki zao msingi.

Nasi tunapenda sana kusimama kidete kulinda na kutetea; uhuru na haki msingi za wanawake, kwa kuhakikisha kwamba; wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika mchakato wa kulinda na kudumisha amani katika ngazi mbalimbali za maisha. Wanawake na wasichana wanaoishi katika maeneo mbalimbali ambayo yameathirika kutokana na migogoro ya kivita kwa muda mrefu, wanakabiliana na hatari kubwa ya manyanyaso ya kijinsia hasa wakati wa kutafuta mahitaji msingi kwa ajili ya familia zao.

Tupige vita manyanyaso na dhuluma dhidi ya wanawake, kwa kulinda na kutetea haki msingi za wanawake kwaajili ya Utu na heshima ya wanawake na binadamu kwa ujumla. Wanawake wakiwezeshwa kiuchumi ni wadau wakuu katika harakati za maendeleo endelevu. Jambo hili linahitaji utendaji mfungamano wa kijamii. Nawapongeza wadau mbalimbali ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba, wanaendeleza mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, nyanyaso za kijinsia, pamoja na kuendeleza kutoa mwono chanya juu ya umuhimu wa jamii kuwawezesha wanawake. Haya ni mapambano endelevu yanayoweza kusaidia kupunguza dhuluma na manyanyaso wanayofanyiwa wanawake.

-NAWAALIKA WADAU WOTE KUUNGANISHA NGUVU ZETU ZA PAMOJA KWA KUWAJIBIKA KIKAMILIFU, ILI KUNG'OA KABISA MANYANYASO NA MADHULUMU DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA.

No comments:

WATEMBELEAJI