Wednesday, February 16, 2011

HAPA MWENDO WA GESI TU...HAKUNA P WALA DIESEL.




FIAT -PANDA; kigari cha kazini kwangu, hapa nikijaza Gesi aina ya METANO. Gesi hii inasaidia sana kupunguza ghalama za mafuta pia kutokuchafua hali ya hewa katika mazingira, pia kupunguza magonjwa mengi kama vile kansa nk. Yanayosababishwa na uchafunzi wa hali ya hewa ya magari kwa moshi, maana moshi wa magari ni sumu mbaya sana.
Kuna Gesi aina mbili ya magari, kuna Metano na GPL. Kwasasa magari mengi sana ni ya gesi, na huduma zimeongezeka za gesi, hapo mwanzo ilikuwa shida sana upatikanaji wa gesi katika vituo vya mafuta. Sasa kila mahali unapata gesi tu! Huwa nikitumia aina nyingine ya gari ya Dizeli ya hapo kazini kwangu, natumia ghalama kubwa sana kwa mafuta, lakini nikitumia hii Panda, utafikiri utani kwa ulaji wa gesi na hela ni ndogo sana labda mara sita yake kwa upungufu wa fedha, safari ni hiyo hiyo na umbali ni huo huo. Shida ya Metano spidi inapungua kidogo unapokuwa unapanda vimilina, maana milina mikubwa hamna kwa kutobolewa kila mahali, lakini ufikapo kwenye mpando unaweza kubadilisha na kuweka Petrol ili uende haraka zaidi, kuna batani unabadili kutoka kwenye Metano unaigeuzia kwenye Petrol. GPL yenyewe ni unakwenda haraka tu hata milimani, lakini pia bei yake inaongezeka kidogo, kwa unafuu wa bei na matumizi ni Metano peke yake. GPL ni sawa kabisa na gesi ya kupikia....mambo ya Tekelinalokuijia haya!
Mbongo lini?




No comments:

WATEMBELEAJI