....Njooni tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba; kwa maana ndiye Mungu wetu.
Ee Bwana, tunakuomba utulinde sisi watoto wako kwa pendo lisilo na mwisho. Na kwa kuwa twategemea tu neema yako ya mbinguni, utuhifadhi daima kwa ulinzi wako.
Ee Mungu wetu, umeumba vitu vyote hivi duniani ili vitusaidie hasa katika unyonge wetu. Tunakuomba utujalie viwe pia Sakramenti ya kutuletea uzima wa milele, tusifuate ya dunia tu! tukakusahau wewe Baba yetu, na kusahau wenzetu wanao hitaji misaada yetu katika maisha yao, ili tuweze kuwasaidia kwa moyo wote bila kunung'unika. Utukumbushe daima....tuwakumbuke wanao hitaji misaada yetu.
- WADAU WANGU WOTE MNAOPITA HAPA KATIKA KURASA HIZI; NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA SANA YENYE AMANI TELE MIOYONI MWENU! NAWAPENDENI SIKU ZOTE!
No comments:
Post a Comment