MH.NCHIMBI APATA AJALI KIBAIGWA - DODOMA!
Habari ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Zelotte Steven...zinasema kwamba Waziri wa Habari Vijana na Utamaduni, Mh.Emmanuel Nchimbi, amepata ajali maeneo ya Kibaigwa Mkoani Dodoma, katika barabara ya Morogoro - Dodoma...kwa gari aliyokua akisafiria kugongana na Basi, wakati akielekea Bungeni mjini Dodoma. Ambapo Bunge linaanza vikao vyake rasmi.Hata hivyo Kamanda Zelotte Steven; amesema hali ya Waziri Nchimbi inaendelea vizuri na ameshawasili Mjini Dodoma ambapo amepumzika. Ajali hiyo ya kawaida tu! japo gari la Mh.Waziri limeharibika sana!
No comments:
Post a Comment