Monday, March 14, 2011

HATMA YA WATANZANIA WAISHIO NJE KUJULIKANA BUNGENI!

Hatma ya Watanzania waishio nje ya nchi inatarajia kujulikana wakati wa kikao cha Bunge lijalo...kikao kinatarajiwa kufanyika Aprili, 2011.
Uraia wa nchi mbili ni moja kati ya masuala yatakayotolewa majibu wakati wa Bunge hilo lijalo. Haya yalielezwa hivi karibuni Jijini Dar es salaam na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa, Mh.Benard Membe....wakati akizungumza kupitia Televisheni ya ITV. Membe ambaye hakuzungumza kwa kina sana swala hili, aliwataka Watanzania kuwa na subira. Kwa mujibu wa Waziri huyo idadi ya Watanzania walioko nje inakadiriwa kufikia kati ya milioni 1.5 hadi 2. ''Bado tunaendelea kuwatambua kwa idadi, lazima tufanye hivyo ili waweze kuleta fedha wanazotengeneza huko nje...kupitia jamaaa zao mbalimbali hatimaye kuleta maendeleo'' ...alisema hivyo Waziri Membe.

No comments:

WATEMBELEAJI