Friday, March 18, 2011

ITALIA YAADHIMISHA MIAKA 150 JANA!

NDEGE ZA KIVITA ZIKIPITA ANGANI KUCHORA RANGI YA BENDERA YA NCHI YA ITALIA HIVYO KUASHIRIA MAADHIMISHO YA MIAKA 150.

Italia imeadhimisha miaka 150 ya Taifa kwa sherehe kubwa nchi nzima, tarehe 17 Machi...ambapo ni kumbukumbu ya tarehe na mwezi kama huo mwaka 1861, mfalme Victor Emanuel wa pili, alipoiunganisha Italia ambayo ilikuwa imegawanyika katika Mikoa minne chini ya udhibiti wa kigeni.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Rais Giorgio Napoletano wa Italia...amesema; iwapo Waitaliano wangeendelea kubaki na utengano huo wangepotezwa na historia na kamwe wasingeweza kuwa moja ya Mataifa yenye nguvu Barani Ulaya.
Hata hivyo Jimbo la Tyrolia lililoko kusini mwa Italia ambako wakazi wake wanazungumza lugha ya Kijerumani, liligoma kushiriki katika sherehe hizo.

No comments:

WATEMBELEAJI