Wednesday, March 16, 2011

JIMBO KATOLIKI JIPYA LA KONDOA - TANZANIA LATANGAZWA!

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameunda Jimbo jipya la Kondoa - Tanzania, kwa kumega Jimbo Katoliki Dodoma, na litakuwa chini ya Jimbo kuu la Dar es salaam. Amemteuwa Mh.Padre Bernardine Mfumbusa, kutoka Jimbo Katoliki Dodoma kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Kondoa.

Jimbo Katoliki Kondoa, linaundwa kutoka katika Wilaya ya Kondoa, lililoko kaskazini mwa Jimbo Katoliki Dodoma, likipakana na Jimbo la Singida, Mbulu, na Jimbo kuu la Arusha. Jimbo Katoliki Kondoa litakuwa na Parokia tisa, zitakazo hudumiwa na mapadre wa Jimbo kumi na tano, mapadre watawa wawili, na watawa wa kike jumla yao ni themanini na saba. Jimbo lina waseminari wawili.

Kila laheri kwa Jimbo jipya la Kondoa.

No comments:

WATEMBELEAJI