Leo ni Jumapili ya kwanza ya kwaresima, tujirekebishe mienendo yetu mibaya kwa kuheshimu kwaresima; katika kipindi hiki tunaalikwa kubadili mienendo yetu kwa kusali zaidi na kuwa na Mungu kwa ukaribu zaidi, kwa kuwaheshimu watu wote, na kufunga kwa kujinyima mambo mbalimbali kwaajili ya kusaidia wale wenzetu wasio na uwezo kabisa.
Ataniita nami....nitamwitikia; atamwokoa na kumtukuza, kwa siku nyingi nitamshibisha.
Mtu hataishi kwa mkate tu! ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Ee Mungu Mwenyezi, utujalie tuzidi kuifahamu siri ya Kristu na kupata manufaa yake katika mwenendo wetu mwema kwa mfungo wa kwaresima wa kila mwaka.
No comments:
Post a Comment