Sunday, May 29, 2011

MANENO MAZURI YA JUMAPILI HII YA 6 YA PASKA!

Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni Bwana amelikomboa taifa lake....aleluya!


Ee Mungu Mwenyezi, utuwezeshe kuadhimisha kwa bidii siku hizi za furaha tunazo zitumia kwa heshima ya Bwana aliyefufuka. Na hayo tunayo yakumbuka sasa, tuyazingatie daima kwa matendo.

Bwana asema; mkinipenda mimi mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele yote.


Ee Mungu Mwenyezi wa milele, wewe watuponya kwa kufufuka kwake Kristu ili tupate uzima wa milele. Utuzidishie neema za fumbo la Paska, na kutujaza mioyoni mwetu nguvu ya chakula hiki cha wokovu.

No comments:

WATEMBELEAJI