Sunday, June 12, 2011

JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NINYI NYOTE WADAU WANGU!



TAFAKARI YANGU YA JUMAPILI HII;


Hakuna aliye mkamilifu wala bora zaidi, sote tuna mapungufu yetu mbele ya Mungu wetu. Si mimi, si wewe, wala yule...aliye safi bila kasoro yoyote, sote tuna mapungufu tu mbele ya Mwenyezi Mungu. Tofauti zetu katika Karama zisitufanye kujivuna sana hata kuwadharau wengine, tofauti zetu za kimaumbile yote ni kwa uwezo wake Mungu...tuyapokee na tumshukuru. Ona wazima, ona wagonjwa, ona viwete, ona matajiri, ona maskini...nao wajinga, sote tumeumbwa kwa sura na mfano wake Mungu. Ona weupe, ona weusi, ona warefu, ona wafupi, ona wanene, ona wembamba.....sote tumeumbwa kwa sura na mfano wake Baba Mungu Mwenyezi. Tuheshimiane, tushirikiane, tusaidiane na tupendane. Ee Mungu Baba twakushukuru sana na utujalie maisha mema na mwisho tupate uzima wa milele, amina!

No comments:

WATEMBELEAJI