Friday, June 24, 2011

MAPAMBANO YA MAISHA YANAENDELEA.......



Maisha ni safari ndefu....ni lazima kupambana na kila vikwanzo, usikate tamaa mapema ni muhimu sana kuwa na subira na mategemeo mengi kwa Mwenyezi Mungu yeye pekee ndiye awezaye kutusaidia kwa kupitia ndugu na jamaa zetu, hivyo kila jambo hatuna budi kumshukuru kwa upendo mkubwa usio na kifani. Nimetumia picha hii kwasababu naipenda, inaonyesha jinsi wafanyakazi wakifurahi, wakati huo huo wakiwa na mafazi yao ya kazi....inabidi tufurahi sana muda wote, wakati wa kazi, wakati wa shida nk....yote ni mapenzi ya Mungu, wadau wangu nawasihi sana msiwe wepesi wa kukata tamaa kwa kila jambo, ni kujituma na kumwomba sana Mwenyezi Mungu. Wakati huo huo ukiendelea kufurahi!

No comments:

WATEMBELEAJI