Friday, June 17, 2011

NYUMBA ZETU ZA UGOGONI HIZI...TOKA ENZI ZA MABABU!

Nyumba zetu za ugogoni hizi (Mbavu za mbwa)....wengine tumekulia humu humu. Ukisema mbaya wenyewe wakikusikia watakupiga kweli kweli, mtu chake bwana!
Nakumbuka marehemu Bibi yangu alijengewa nyumba nzuri ya kuezekwa kwa bati, alijegewa na wanawe, alikaa wiki moja tu! akashindwa na kusema; mvua ikinyesha kelele sana, mara joto sana hawezi kulala...na sababu kedekede, wao wamezoea sana hizi nyumba. Wewe unaweza sema mbaya hazina hathi kabisa nk....lakini wao ni nyumba za kifahari sana.

No comments:

WATEMBELEAJI