Monday, July 11, 2011

HII KALI......

Mme karudi nyumbani akiwa njwii (kalewa). Mke akamwuliza; Mme wangu mbona umelewa hivi, twende unionyeshe ulikuwa unakunywa wapi. Mme akampeleka kwenye baa ya muuza gongo. Mama muuza gongo akasema; kweli mme wako alikuwa hapa akipata kilaji. Mke kwa hasira akamwambia; siku ambayo utatia miguu yako hapa nitakuacha! Mme akamwomba msamaha kuwa; hatatia miguu yake hapo kwenye baa tena. Kesho yake mama muuza baa alimwona yule baba akiingia kwa mikono na miguu juu, akamwuliza; kulikoni? Mzee wa watu akajibu; wewe umesahau kuwa jana nilimwahidi mke wangu kuwa sita tia miguu hapa, sasa nimekuja kwa mikono, mwenzio sitaki kuachika.

No comments:

WATEMBELEAJI