Wednesday, September 28, 2011

DAWA YA MATATIZO NI KUYATATUA!

Dawa ya matatizo ni kuyatatua.....si kuyakimbia!
Hata kama unaona aibu kwa matatizo yako, lakini dawa ya matatizo ni kuyatatua. Najua kabisa kuwa kuna matatizo mengine ni mazito sana na ni ya aibu sana, lakini sio uyakimbie ni lazima uyakabili ili uyamalize hayo matatizo, la sivyo yatakuandama daima! Ona aibu lakini usipitilize kiasi kwamba usiyakabili matatizo yako, tafuta namna ya kuyatatua na ukisha yatatua usirudie tena kutenda hayo uliyo tenda. Pia usisite ushauri wa mtu anayekushauri kwa mema ili uweze kuyatatua hayo matatizo. Usisite ushauri....shaurika, changanya na mawazo yako ili utatue matatizo yako. Kama unaona ushauri wa mwenzio haukufai....utupilie mbali, fata ya kwako...ila unapopewa ushauri sikiliza kwa makini, halafu chekecha kisha uchague kwa makini. Wewe pekee ndiwe unayeweza kuamua.

-Tatua matatizo yako mapema, ili uyamalize mapema....la sivyo yatazidi kuwa mazito daima!

1 comment:

WATEMBELEAJI